The Bible › Biblia Takatifu › 1 Samuel 21

1 Samuel 21:10

Daudi aliamka na kukimbia mbali na Sauli na akaenda kwa Akishi, mfalme wa Gathi.

1 Samuel 21:10 · Biblia Takatifu

← PreviousRead 1 Samuel 21Next →

1 Samuel 21:10 in other translations

KJV King James Version

And David arose, and fled that day for fear of Saul, and went to Achish the king of Gath.

BSB Berean Standard Bible

That day David fled from Saul and went to Achish king of Gath.

WEB World English Bible

David arose and fled that day for fear of Saul, and went to Achish the king of Gath.

Every translation above is public domain and free to share. Other versions — NIV · ESV · NKJV · NLT · NASB · CSB · AMP — are copyrighted and open on their publishers’ partner site.

In context

7 Basi siku hiyo mmoja wa watumishi wa Sauli alikuwapo mahali hapo, ameshilkiliwa mbele za BWANA. Jina la mtu huyo aliitwa Doegi Mwedomu, mkuu wa wachungaji wa Sauli.

8 Daudi akamwambia Ahimeleki, “Je, hakuna hata mkuki wowote au upanga? Maana mimi sikubeba upanga wangu wala silaha zangu, maana ile shughuli ya mfalme ilikuwa ya muhimu.”

9 Kuhani akasema, “Ule upanga wa Mfilisti Goliathi, uliyemuua katika bonde la Ela, uko hapa umefunikwa katika nguo nyuma ya naivera. kama unataka kuuchukua huo, uchukue, maana hakuna silaha nyingine hapa.” Daudi akasema, “Hakuna silaha nyingine kama hiyo, nipatie hiyo.”

10 Daudi aliamka na kukimbia mbali na Sauli na akaenda kwa Akishi, mfalme wa Gathi.

11 Mtumishi wa Akishi akamwambia, “huyu siye Daudi mfalme wa nchi hii? Je, wanawake hawakupokezana wakiimba na kucheza, 'Sauli ameua maelfu yake, na Daudi makumi elfu yake?”'

12 Daudi akayaweka maneno hayo moyoni mwake na akamwogopa sana Akishi, mfalme wa Gathi.

13 Daudi akabadili mwenendo wake mbele yao na akajifanya kuwa mwendawazimu machoni pao; akachora-chora alama kwenye vizingiti vya milango huku akitiririsha mate yake chini ya ndevu zake.

Read 1 Samuel 21 in the app The whole chapter

Search the Scriptures

Choose a translation

KJVBSBWEBNHEBASVYLTDBYWBTBBEEBRGNVDRALUTCANRIVLSGRVABPMYORIGBSWATGLIRV