The Bible › Biblia Takatifu › Mark 12

Mark 12:41

Kisha Yesu aliketi chini karibu na sanduku la sadaka ndani ya eneo la hekalu; alikuwa akitazama watu waliokuwa wakitia pesa zao ndani ya sanduku. Watu wengi matajiri waliweka kiasi kikubwa cha pesa.

Mark 12:41 · Biblia Takatifu

← PreviousRead Mark 12Next →

Mark 12:41 in other translations

KJV King James Version

And Jesus sat over against the treasury, and beheld how the people cast money into the treasury: and many that were rich cast in much.

BSB Berean Standard Bible

As Jesus was sitting opposite the treasury, He watched the crowd putting money into it. And many rich people put in large amounts.

WEB World English Bible

Jesus sat down opposite the treasury and saw how the multitude cast money into the treasury. Many who were rich cast in much.

Every translation above is public domain and free to share. Other versions — NIV · ESV · NKJV · NLT · NASB · CSB · AMP — are copyrighted and open on their publishers’ partner site.

In context

38 Katika mafundisho yake Yesu alisema, “Jihadharini na waandishi, wanaotamani kutembea na kanzu ndefu na kusalimiwa kwenye masoko

39 na kuketi kwenye viti vya wakuu katika masinagogi na katika sikukuu kwa maeneo ya wakuu.

40 Pia wanakula nyumba za wajane na wanaomba maombi marefu ili watu wawaone. Hawa watu watapokea hukumu iliyo kuu.”

41 Kisha Yesu aliketi chini karibu na sanduku la sadaka ndani ya eneo la hekalu; alikuwa akitazama watu waliokuwa wakitia pesa zao ndani ya sanduku. Watu wengi matajiri waliweka kiasi kikubwa cha pesa.

42 Kisha mwanamke mjane maskini alikuja na kutia vipande viwili, thamani ya senti.

43 Kisha akawaita wanafunzi wake na kuwaambia, “Amini nawaambia, mwanamke huyu mjane ametia kiasi kikubwa zaidi ya wote ambao wameshatoa katika sanduku la sadaka.

44 Kwani wote wametoa kutokana na wingi wa mapato yao. Lakini mwanamke mjane huyu, kutoka katika umaskini wake, katia pesa yote ambayo alipaswa kuitumia kwa maisha yake.”

Read Mark 12 in the app The whole chapter

Search the Scriptures

Choose a translation

KJVBSBWEBNHEBASVYLTDBYWBTBBEEBRGNVDRALUTCANRIVLSGRVABPMYORIGBSWATGLIRV