The Bible › Biblia Takatifu › Mark 12
Yeye si Mungu wa wafu, bali wa walio hai. Ni dhahiri mmepotoka.”
Mark 12:27 · Biblia Takatifu
He is not the God of the dead, but the God of the living: ye therefore do greatly err.
He is not the God of the dead, but of the living. You are badly mistaken!”
He is not the God of the dead, but of the living. You are therefore badly mistaken.”
Every translation above is public domain and free to share. Other versions — NIV · ESV · NKJV · NLT · NASB · CSB · AMP — are copyrighted and open on their publishers’ partner site.
24 Yesu aliwaambia, “Je! Hii si sababu kuwa mmepotoshwa, kwa sababu hamjui maandiko wala nguvu za Mungu?”
25 Wakati wa kufufuka toka kwa wafu, hawataoa wala kuingia katika ndoa, bali watakuwa kama malaika wa mbinguni.
26 Lakini, kuhusu wafu ambao wanafufuliwa, Je! Hamkusoma kutoka katika kitabu cha Musa, katika habari za kichaka, jinsi Mungu alivyosema na kumwambia, 'Mimi ni Mungu wa Abrahimu, na Mungu wa Isaka, na Mungu wa Yakobo?'
27 Yeye si Mungu wa wafu, bali wa walio hai. Ni dhahiri mmepotoka.”
28 Mmoja wa waandishi alikuja na kuyasikia mazungumzo yao; aliona kwamba Yesu aliwajibu vema. Alimwuliza, “Je! ni amri ipi iliyo ya muhimu zaidi katika zote?”
29 Yesu alimjibu, “Iliyo ya muhimu ni hii, “Sikia, Israeli, Bwana Mungu wetu, Bwana ni mmoja.
30 Lazima umpende Bwana Mungu wako, kwa moyo wako yote, kwa roho yako yote, kwa akili yako yote, na kwa nguvu zako zote.'
Read Mark 12 in the app The whole chapter