The Bible › Biblia Takatifu › Mark 12
Kisha wa pili alimchukua naye akafa, hakuacha watoto. Na wa tatu hali kadhalika.
Mark 12:21 · Biblia Takatifu
And the second took her, and died, neither left he any seed: and the third likewise.
Then the second one married the widow, but he also died and left no children. And the third did likewise.
The second took her, and died, leaving no children behind him. The third likewise;
Every translation above is public domain and free to share. Other versions — NIV · ESV · NKJV · NLT · NASB · CSB · AMP — are copyrighted and open on their publishers’ partner site.
18 Kisha Masadukayo, wasemao hakuna ufufuo, walimwendea. Wakamuwuliza, wakisema,
19 “Mwalimu, Musa alituandikia kuwa, 'Ikiwa ndugu ya mtu akifa na kumwacha mke nyuma yake, lakini hakuacha mtoto, mtu atamchukua mke wa ndugu yake, na kujipatia watoto kwa ajili ya ndugu yake.'
20 Kulikuwa na ndugu saba, wa kwanza alitwaa mke na kisha akafa, hakuacha watoto.
21 Kisha wa pili alimchukua naye akafa, hakuacha watoto. Na wa tatu hali kadhalika.
22 Na wa saba alikufa bila kuacha watoto. Mwishowe na mwanamke pia akafa.
23 Wakati wa ufufuo, watakapofufuka tena, Je! Atakuwa mke wa nani? Kwani wale ndugu wote saba walikuwa waume wake.”
24 Yesu aliwaambia, “Je! Hii si sababu kuwa mmepotoshwa, kwa sababu hamjui maandiko wala nguvu za Mungu?”
Read Mark 12 in the app The whole chapter