The Bible › Biblia Takatifu › Leviticus 21
mtu mwenye kibiongo mgongoni mwake au aliye na kimo kidogo au wembamba usio wa kawaida, au mtu mwenye kasoro machoni mwake, au mwenye ugonjwa, kidonda, upele, au yule ambaye korodani zake zimeharibiwa.
Leviticus 21:20 · Biblia Takatifu
← PreviousRead Leviticus 21Next →
Or crookbackt, or a dwarf, or that hath a blemish in his eye, or be scurvy, or scabbed, or hath his stones broken;
or who is a hunchback or dwarf, or who has an eye defect, a festering rash, scabs, or a crushed testicle.
or hunchbacked, or a dwarf, or one who has a defect in his eye, or an itching disease, or scabs, or who has damaged testicles.
Every translation above is public domain and free to share. Other versions — NIV · ESV · NKJV · NLT · NASB · CSB · AMP — are copyrighted and open on their publishers’ partner site.
17 Zungumza na Aroni na umwambie, 'mtu yeyote wa ukoo wako katika vizazi vyako vyote mwenye kasoro mwilini mwake, asisogee kutoa chakula kwa Mungu wake.
18 Mtu yeyote mwenye kasoro mwilini mwake asimkaribie Yahweh,
19 mtu kama vile: kipofu au mtu asiyeweza kutembea, mtu aliyeharibiwa uso au kupungukiwa na viungo mwilini, mtu aliye na mguu au mkono wenye ulemavu,
20 mtu mwenye kibiongo mgongoni mwake au aliye na kimo kidogo au wembamba usio wa kawaida, au mtu mwenye kasoro machoni mwake, au mwenye ugonjwa, kidonda, upele, au yule ambaye korodani zake zimeharibiwa.
21 Hakutakuwa na mtu miongoni mwa ukoo wa Aroni kuhani mkuu mwenye kasoro mwilini atakayekaribia kutoa matoleo yatakayoteketezwa kwa moto kwa ajili ya Yahweh. Mtu kama huyo mwenye kasoro mwilini hatakaribia ili kutoa mkate wa Mungu wake.
22 Anaweza kula chakula cha Mungu wake, ama iwe baadhi ya vile vilivyo vitakatifu sana au vile vitakatifu.
23 Hata hivyo, hataingia ndani ya pazia wala kuisogelea madhabahu, kwa sababu ana kasoro mwilini mwake, ili kwamba asipanajisi mahali patakatifu pangu, kwa kuwa Mimi ndimi Yahweh anayewafanya watakatifu.”
Read Leviticus 21 in the app The whole chapter