The Bible › Biblia Takatifu › Leviticus 13
Naye kuhani atamchunga tena katika siku ya saba ili kuona kama ugonjwa ubepona na haujasambaa zaidi kwenye ngozi. kama haujasambaa, basi, kuhani atamtangaza kuwa yeye ni safi. Ni upele tu. Naye atafua nguo zake, na kisha yeye yu safi.
Leviticus 13:6 · Biblia Takatifu
← PreviousRead Leviticus 13Next →
And the priest shall look on him again the seventh day: and, behold, if the plague be somewhat dark, and the plague spread not in the skin, the priest shall pronounce him clean: it is but a scab: and he shall wash his clothes, and be clean.
The priest will examine him again on the seventh day, and if the sore has faded and has not spread on the skin, the priest shall pronounce him clean; it is a rash. The person must wash his clothes and be clean.
The priest shall examine him again on the seventh day. Behold, if the plague has faded and the plague hasn’t spread in the skin, then the priest shall pronounce him clean. It is a scab. He shall wash his clothes, and be clean.
Every translation above is public domain and free to share. Other versions — NIV · ESV · NKJV · NLT · NASB · CSB · AMP — are copyrighted and open on their publishers’ partner site.
3 Naye kuhanai atachunguza ugonjwa huo kwenye ngozi ya mwili wake. Iwapo malaika zilizopo eneo lenye ugonjwa zimegeuka kuwa nyeupe, na iwapo ugonjwa umejitokeza juu ya ngozi, huo ni ugonjwa wa kuambukiza. Baada cha kuhani kumchunguza, atamtangaza kuwa ni najisi.
4 Iwapo lile doa ling'aalo katika ngozi yake ni jeupe, na kuonekana kwake halikwenda chini zaidi ya ngozi, na iwapo malaika za eneo lenye ugonjwa hazijabadilika kuwa nyeupe, naye kuhani atamtenga mgonjwa kwa siku saba.
5 Katika siku ya saba, huyo kuhani itambidi kumchunguza tena ili kuona kama katika maamzi yake huo ugonjwa siyo mbaya, na kama haujaenea kwenye ngozi. Iwapo haujaenea, basi, kuhani atamtenga kwa siku saba zaidi.
6 Naye kuhani atamchunga tena katika siku ya saba ili kuona kama ugonjwa ubepona na haujasambaa zaidi kwenye ngozi. kama haujasambaa, basi, kuhani atamtangaza kuwa yeye ni safi. Ni upele tu. Naye atafua nguo zake, na kisha yeye yu safi.
7 Lakini endapo ule upele utakuwa umishasambaa kwenye ngozi baada ya kuwa amejionyesha kwa kuhani kwa ajili kusafishwa kwake, itambidi kujionyesha tena kwa kuhani.
8 Naye kuhani atamchunguza ilikuona kama huo upele umsambaa zaidi ndani ya ngozi. Na endapo utakuwa umesambaa, kisha kuhani atamtangaza kuwa najisi. Huo ni ugonjwa wa kuambukiza.
9 Iwapo ugonjwa wa ngozi wa kuambukiza umo kwa mtu fulani, naye mtu huyo yapasa aletwe kwa kuhan.
Read Leviticus 13 in the app The whole chapter