The Bible › Biblia Takatifu › Joshua 21
Upigaji wa kura kwa ajili ya koo za Wakohathi ulileta matokeo haya: makuhani ambao ni wazawa wa Haruni ambao walitokana na Walawi, walipokea miji kumi na mitatu waliopewa kutoka kwa kabila la Yuda, kutoka kabila la Simoni, na kutoka kabila la Benyamini.
Joshua 21:4 · Biblia Takatifu
← PreviousRead Joshua 21Next →
And the lot came out for the families of the Kohathites: and the children of Aaron the priest, which were of the Levites, had by lot out of the tribe of Judah, and out of the tribe of Simeon, and out of the tribe of Benjamin, thirteen cities.
The first lot came out for the Kohathite clans. The Levites who were descendants of Aaron the priest received thirteen cities by lot from the tribes of Judah, Simeon, and Benjamin.
The lot came out for the families of the Kohathites. The children of Aaron the priest, who were of the Levites, had thirteen cities by lot out of the tribe of Judah, out of the tribe of the Simeonites, and out of the tribe of Benjamin.
Every translation above is public domain and free to share. Other versions — NIV · ESV · NKJV · NLT · NASB · CSB · AMP — are copyrighted and open on their publishers’ partner site.
1 Kisha wakuu wa koo za Walawi walimwendea Eliazari kuhani, na kwa Yoshua mwana wa Nuni, na kwa viongozi wa familia za mababu zao miongoni mwa watu wa Israeli.
2 Waliwaambia, “Yahweh aliwaagizeni ninyi kwa mkono wa Musa kwamba mtupatieni miji ya kuishi yenye maeneo kwa ajili ya kuchungia ya mifugo.” waliyasema haya huko Shilo katika nchi ya Kanaani.
3 Hivyo, kwa agizo la Yahweh, watu wa Israeli waliwapa Walawi kutoka katika urithi wa wao miji ifuatayo pamoja na maeneo yao ya kuchungia.
4 Upigaji wa kura kwa ajili ya koo za Wakohathi ulileta matokeo haya: makuhani ambao ni wazawa wa Haruni ambao walitokana na Walawi, walipokea miji kumi na mitatu waliopewa kutoka kwa kabila la Yuda, kutoka kabila la Simoni, na kutoka kabila la Benyamini.
5 Koo zilizobaki za Wakohathi walipokea kwa kupiga kura kwa miji kumi kutoka katika kabila za Efraimu, Dani, na kutoka kwa nusu ya kabila la Manase.
6 Na watu wazawa wa Gershoni walipewa miji kumi na mitatu kwa kupigiwa kura kutoka kwa koo za kabila la Isakari, Asheri, Nafutali, na nusu ya kabila la Manase katika Bashani.
7 Watu waliokuwa wazawa wa Merari walipokea miji kumi na miwili kutoka katika makabila ya Rubeni, Gadi na Zabuloni.
Read Joshua 21 in the app The whole chapter