The Bible › Biblia Takatifu › John 17
Huu ndio uzima wa milele: kwamba wakujue wewe, Mungu wa kweli na wa pekee, na yeye uliyemtuma, Yesu Kristo.
John 17:3 · Biblia Takatifu
And this is life eternal, that they might know thee the only true God, and Jesus Christ, whom thou hast sent.
Now this is eternal life, that they may know You, the only true God, and Jesus Christ, whom You have sent.
This is eternal life, that they should know you, the only true God, and him whom you sent, Jesus Christ.
Every translation above is public domain and free to share. Other versions — NIV · ESV · NKJV · NLT · NASB · CSB · AMP — are copyrighted and open on their publishers’ partner site.
1 Yesu aliyasema mambo haya; kisha akainua macho yake kuelelea mbinguni na akasema, “Baba, saa imewadia; mtukuze mwanao ili na mwana naye akutukuze wewe -
2 kama vile ulivyompatia mamlaka juu ya vyote vyenye mwili ili awape uzima wa milele wale wote uliompatia.
3 Huu ndio uzima wa milele: kwamba wakujue wewe, Mungu wa kweli na wa pekee, na yeye uliyemtuma, Yesu Kristo.
4 Nilikutukuza hapa duniani, na kuikamilisha kazi uliyonipa niifanye.
5 Sasa, Baba, unitukuze mimi pamoja na wewe mwenyewe kwa utukufu ule niliokuwa nao pamoja na wewe kabla ya ulimwengu kuumbwa.
6 Nililifunua jina lako kwa watu ulionipa hapa duniani. Walikuwa watu wako; lakini ulinikabidhi mimi. nao wamelishika neno lako.
Read John 17 in the app The whole chapter