The Bible › Biblia Takatifu › Daniel 8
Alizidi kuwa mkubwa, mkubwa kama kamanda wa jeshi la kimungu. Sadaka za kuteketezwa za kila siku ziliondolewa mbali na yeye, na sehemu yake takatifu zilitiwa unajisi.
Daniel 8:11 · Biblia Takatifu
Yea, he magnified himself even to the prince of the host, and by him the daily sacrifice was taken away, and the place of his sanctuary was cast down.
It magnified itself, even to the Prince of the host; it removed His daily sacrifice and overthrew the place of His sanctuary.
Yes, it magnified itself, even to the prince of the army; and it took away from him the continual burnt offering, and the place of his sanctuary was cast down.
Every translation above is public domain and free to share. Other versions — NIV · ESV · NKJV · NLT · NASB · CSB · AMP — are copyrighted and open on their publishers’ partner site.
8 Ndipo mbuzi alikua akawa mkubwa, lakini alipokuwa na nguvu, pembe kubwa ilivunjwa, na katika sehemu yake zilichipuka na kukua pembe nne kubwa zilizochomoza kuelekea pepo nne za mbingu.
9 Kutoka katika pembe moja ilichipuka pembe nyingine, ilikuwa ndogo hapo awali, lakini baadaye ilikuwa pembe kubwa upande wa kusini, na mashariki, na katika nchi ya uzuri.
10 Pembe ilikuwa kubwa na matokeo yake iliinua vita dhidi ya jeshi la mbinguni. Baadhi ya jeshi na nyota kadhaa zilitupwa chini duniani, na zilikanyagwa.
11 Alizidi kuwa mkubwa, mkubwa kama kamanda wa jeshi la kimungu. Sadaka za kuteketezwa za kila siku ziliondolewa mbali na yeye, na sehemu yake takatifu zilitiwa unajisi.
12 Kwasababu ya uasi, pembe ya mbuzi ilipewa jeshi, na sadaka za kuteketezwa zitasitishwa. Pembe itautupa ukweli chini ardhini, na itafanikiwa katika kila jambo ilifanyalo.
13 Kisha nilimsikia mtakatifu mmoja akiongea na mtakatifu mwingine akamjibu, “ Mambo haya yatadumu kwa muda gani, maono haya ya sadaka ya kuteketezwa, dhambi ile iletayo uharibifu, ukabidhiajia wa sehemu takatifu, na jeshi la mbinguni kukanyagwa?
14 Aliniambia, “ Itadumu kwa jioni na asubuhi zipatazo 2, 300. Baada ya hapo, mahali patakatifu patawekwa sawa.”
Read Daniel 8 in the app The whole chapter