The Bible › Biblia Takatifu › Daniel 7

Daniel 7:23

Hiki ndicho mtu yule alichokisema, 'Kwa habari ya mnyama wanne, utakuwa ni ufalme wa nne juu ya dunia ambao utakuwa tofauti na falme zingine zote. Utaimeza dunia yote, na utaikanyaga yote chini na kuivunja vunja vipande vipande.

Daniel 7:23 · Biblia Takatifu

← PreviousRead Daniel 7Next →

Daniel 7:23 in other translations

KJV King James Version

Thus he said, The fourth beast shall be the fourth kingdom upon earth, which shall be diverse from all kingdoms, and shall devour the whole earth, and shall tread it down, and break it in pieces.

BSB Berean Standard Bible

This is what he said: ‘The fourth beast is a fourth kingdom that will appear on the earth, different from all the other kingdoms, and it will devour the whole earth, trample it down, and crush it.

WEB World English Bible

“So he said, ‘The fourth animal will be a fourth kingdom on earth, which will be different from all the kingdoms, and will devour the whole earth, and will tread it down and break it in pieces.

Every translation above is public domain and free to share. Other versions — NIV · ESV · NKJV · NLT · NASB · CSB · AMP — are copyrighted and open on their publishers’ partner site.

In context

20 Nilitaka kujua juu ya pembe kumi katika kichwa chake, na kuhusu pembe nyingine iliyochomoza, na ambayo mbele yake pembe zingine tatu zilianguka chini. Nilitaka kujua kuhusu pembe yenye macho na kuhusu mdomo uliokuwa unajisifu kwa mambo makubwa na ambayo ilionekana kuwa ni kubwa kuliko zingine.

21 Na nilipotazama, pembe hii iliinua vita dhidi ya watu watakatifu na ilikuwa inawawashinda mpaka pale

22 Mzee wa Siku alipokuja, na watu watakatifu wa Mungu Aliye Juu Sana. Ndipo wakati ulipowadia ambapo watu watakatifu waliupokea ufalme.

23 Hiki ndicho mtu yule alichokisema, 'Kwa habari ya mnyama wanne, utakuwa ni ufalme wa nne juu ya dunia ambao utakuwa tofauti na falme zingine zote. Utaimeza dunia yote, na utaikanyaga yote chini na kuivunja vunja vipande vipande.

24 Na kuhusu pembe kumi, kutoka katika ufalme huu, wafalme kumi watainuka, na mwingine atainuka baada yao. Atakuwa wa tofauti na wale waliomtangulia, na atawashinda wale wafalme watatu.

25 Atazungumza maneno kinyume cha Yeye Aliye Juu sana na atawatesa watu watakatifu wa Mungu Aliye Juu. Atajaribu kuzibadili sikukuu na sheria. Mambo haya atapewa mikononi mwake kwa mwaka mmoja, miaka miwili na nusu mwaka.

26 Lakini kikao cha mahakama kitaitishwa, na watazichukua nguvu zake za kifalme ili mwisho aweza kuharibiwa na kuteketezwa.

Read Daniel 7 in the app The whole chapter

Search the Scriptures

Choose a translation

KJVBSBWEBNHEBASVYLTDBYWBTBBEEBRGNVDRALUTCANRIVLSGRVABPMYORIGBSWATGLIRV