The Bible › Biblia Takatifu › Daniel 7

Daniel 7:12

Na kwa wale wanyama wanne waliosalia, mamlaka yao yalitwaliwa mbali, lakini maisha yao yaliendelezea kwa kipindi fulani cha muda.

Daniel 7:12 · Biblia Takatifu

← PreviousRead Daniel 7Next →

Daniel 7:12 in other translations

KJV King James Version

As concerning the rest of the beasts, they had their dominion taken away: yet their lives were prolonged for a season and time.

BSB Berean Standard Bible

As for the rest of the beasts, their dominion was removed, but they were granted an extension of life for a season and a time.

WEB World English Bible

As for the rest of the animals, their dominion was taken away; yet their lives were prolonged for a season and a time.

Every translation above is public domain and free to share. Other versions — NIV · ESV · NKJV · NLT · NASB · CSB · AMP — are copyrighted and open on their publishers’ partner site.

In context

9 Na nilipotazama, viti vya enzi vilikuwa vimewekwa, na Mtu wa siku za kale alikaa sehemu yake. Mavazi yake yalikuwa meupe kama theruji, na nywele zake katika kichwa chake zilikuwa safi kama sufu. Kiti chake cha enzi kilikuwa na miali ya moto, na magurudumu yake yalikuwa yanawaka moto.

10 Mto wa moto ulitiririka kutoka mbele yake, na mamilioni ya watu walimtumikia, na wengine mia moja milioni walikuwa wamesimama mbele yake. Na mahakama iliitishwa, na vitabu vilifunguliwa.

11 Niliendelea kuangalia kwasababu ya maneno ya kiburi yaliyosemwa na pembe. Nilitazama wakati mnyama anauliwa, na mwili wake uliharibiwa, na ulitolewa kwa ajili ya kuchomwa moto.

12 Na kwa wale wanyama wanne waliosalia, mamlaka yao yalitwaliwa mbali, lakini maisha yao yaliendelezea kwa kipindi fulani cha muda.

13 Katika maono yangu usiku ule, nilimwona mtu mmoja anakuja katika mawingu ya mbinguni alikuwa kama mwana wa mtu; alikuja kwa Mzee wa Siku na aliletwa mbele zake.

14 Naye alipewa mamlaka ya kiutawala na utukufu na mamlaka ya kifalme ili kwamba watu wote, na mataifa na lugha ziweze kumtumikia yeye. Mamlaka yake ya kutawala ni mamlaka ya milele ambayo hayatapita, na ufalme wake ni ule ambao hautaangamizwa.

15 Na kwangu mimi, Danieli, roho yangu ilihuzunishwa ndani yangu, na maono niliyoyaona katika akili zangu yalinisumbua.

Read Daniel 7 in the app The whole chapter

Search the Scriptures

Choose a translation

KJVBSBWEBNHEBASVYLTDBYWBTBBEEBRGNVDRALUTCANRIVLSGRVABPMYORIGBSWATGLIRV