The Bible › Biblia Takatifu › Daniel 5

Daniel 5:22

Wewe mwana wake, Belshaza, haujaunyenyekeza moyo wako, ingawa aliyajua haya yote.

Daniel 5:22 · Biblia Takatifu

← PreviousRead Daniel 5Next →

Daniel 5:22 in other translations

KJV King James Version

And thou his son, O Belshazzar, hast not humbled thine heart, though thou knewest all this;

BSB Berean Standard Bible

But you his son, O Belshazzar, have not humbled your heart, even though you knew all this.

WEB World English Bible

“You, his son, Belshazzar, have not humbled your heart, though you knew all this,

Every translation above is public domain and free to share. Other versions — NIV · ESV · NKJV · NLT · NASB · CSB · AMP — are copyrighted and open on their publishers’ partner site.

In context

19 Na kwasababu ya ukuu huo, Mungu alimpa watu wote, mataifa, na lugha walimtetemekea na kumwogopa. Aliwauwa wale aliotaka wafe na aliwaacha hai wale aliotaka waishi. Aliwainua wale aliowataka, na aliwashusha wale aliowataka.

20 Lakini wakati moyo ulipokuwa na kiburi na roho yake ilifanywa kuwa mgumu na kwasababu hiyo alitenda kwa kiburi, alishushwa kutoka kiti chake cha enzi cha kifalme, na waliiondoa enzi yake.

21 Aliondolewa katika ubinadamu, alikuwa na akili za mnyama, na aliishi na punda wa mwituni. Alikula majani kama ng'ombe. Mwili wake ulilowanishwa kwa umande wa kutoka mbinguni mpaka pale alipojifunza kwamba Mungu Aliye Juu anatawala juu ya falme za watu na ya kwamba humweka mtu yeyote amtakaye juu yake.

22 Wewe mwana wake, Belshaza, haujaunyenyekeza moyo wako, ingawa aliyajua haya yote.

23 Umejiinua mwenyewe kinyume cha Bwana wa mbinguni. Katika nyumba yake walikuletea vyombo ambavyo wewe, wakuu wako, wake zako na masuria wako walivinywea, na kisha ukaisifia sana sanamu zilitengenezwa kwa fedha na dhahabu, shaba, chuma, mbao, na mawe - sanamu ambazo haziwezi kuona, kusikia wa kujua kitu chochote. Haujamheshimu Mungu ambaye anaishikilia pumzi yako katika mkono wake na ambaye anazijua njia zako zote.

24 Ndipo Mungu aliutuma mkono kutoka katika makao yake na maandishi haya yaliandikwa.

25 Haya ndiyo maandishi ambayo yaliandikwa: 'Mene, Mene, Tekeli na Peresin.'

Read Daniel 5 in the app The whole chapter

Search the Scriptures

Choose a translation

KJVBSBWEBNHEBASVYLTDBYWBTBBEEBRGNVDRALUTCANRIVLSGRVABPMYORIGBSWATGLIRV