The Bible › Biblia Takatifu › Daniel 5
Nimesikia habari kukuhusu wewe, kwamba roho ya miungu iko ndani yako, na ya kwamba mwanga na ufahamu na hekima bora inapatikana ndani yako.
Daniel 5:14 · Biblia Takatifu
I have even heard of thee, that the spirit of the gods is in thee, and that light and understanding and excellent wisdom is found in thee.
I have heard that the spirit of the gods is in you, and that you have insight, intelligence, and extraordinary wisdom.
I have heard of you, that the spirit of the gods is in you and that light, understanding, and excellent wisdom are found in you.
Every translation above is public domain and free to share. Other versions — NIV · ESV · NKJV · NLT · NASB · CSB · AMP — are copyrighted and open on their publishers’ partner site.
11 Kuna mtu katika ufalme wako ambaye ana roho ya miungu watakatifu dani yake. Katika siku za baba yako, mwanga na weledi na hekima ya miungu ilipatikana ndani yake. Mfalme Nebukadneza, baba yako mfalme, alimfanya kuwa mkuu wa waganga, pamoja na mkuu wa wale wanazungumza na wafu, na wa wenye hekima, na wa wataalamu wa nyota.
12 Roho bora, ufahamu, weledi, kutafsiri ndoto, kufafanua mafumbo na kutatua matatizo - hizi ni sifa zilizopatikana kwa mtu huyu Danieli, ambaye mfalme alimwita Belteshaza. Sasa mwiteni Danieli naye atawaambia maana ya kile kilichoandikwa.”
13 Ndipo Danieli alipoletwa mbele ya mfalme. Mfalme akamwambia, “Wewe ni yule Danieli, mmoja kati ya watu wa mateka wa Yuda, ambao baba yangu mfalme aliwaleta kutoka Yuda.
14 Nimesikia habari kukuhusu wewe, kwamba roho ya miungu iko ndani yako, na ya kwamba mwanga na ufahamu na hekima bora inapatikana ndani yako.
15 Na sasa watu wanaojulikana kwa hekima na wale wanaozungumza na wafu, wamekwisha kuletwa mbele yangu, ili kusoma maandishi haya na kunijulisha maana ya tafsiri yake, lakini hawakuweza kunijulisha tafsiri yake.
16 Nimesikia kwamba unaweza kutoa tafsiri na kutatua matatizo. Sasa kama utaweza kusoma maandishi na kuniambia maana yake, utavikwa nguo za zambarau na kuwa na kuvalishwa mkufu wa dhahabu shingoni mwako, na utakuwa mtawala wa tatu mwenye mamlaka katika ufalme.”
17 Kisha Danieli akajibu mbele ya mfalme, “Zawadi yako na iwe kwa ajili yako mwenyewe, na thawabu yako na umpe mtu mwingine. Hata hivyo, mfalme, nitakusomea maandishi na nitakwaambia maana.
Read Daniel 5 in the app The whole chapter