The Bible › Biblia Takatifu › Daniel 4

Daniel 4:16

Akili yake na ibadilishwe kutoka akili ya kibinadamu, na apewe akili ya mnyama mpaka ipite miaka saba.

Daniel 4:16 · Biblia Takatifu

← PreviousRead Daniel 4Next →

Daniel 4:16 in other translations

KJV King James Version

Let his heart be changed from man's, and let a beast's heart be given unto him; and let seven times pass over him.

BSB Berean Standard Bible

Let his mind be changed from that of a man, and let him be given the mind of a beast till seven times pass him by.

WEB World English Bible

Let his heart be changed from man’s, and let an animal’s heart be given to him. Then let seven times pass over him.

Every translation above is public domain and free to share. Other versions — NIV · ESV · NKJV · NLT · NASB · CSB · AMP — are copyrighted and open on their publishers’ partner site.

In context

13 Nilipokuwa nimelala kitandani kwangu, niliona katika akili zangu, mjumbe mtakatifu alishuka kutoka mbinguni.

14 Alipiga kelele na kusema, 'Ukateni mti na yafyekeni matawi yake, yapukutisheni majani yake, na kuyasambaza matunda yake. Wanyama na wakimbie kutoka chini yake na ndege wapae mbali kutoka katika matawi yake.

15 Mkiache kisiki cha mizizi yake katika nchi, mkifunge na fungu la chuma na shaba, katikati ya mche mororo wa shambani. Na kilowanishwe na umande wa kutoka mbinguni. Kiacheni kiishi na wanyama kati ya mimea ya ardhini.

16 Akili yake na ibadilishwe kutoka akili ya kibinadamu, na apewe akili ya mnyama mpaka ipite miaka saba.

17 Uamuzi huu ni kutokana na amri iliyotolewa na mjumbe. Ni uamuzi uliofanya na yeye aliye mtakatifu ili kwamba hao walio hai wajue kwamba Mungu aliye juu sana anatawala juu ya falme za watu na huwapa kwa kila mmoja apendaye kumweka juu yao, hata kwa watu wale wanyenyekevu sana.'

18 Mimi, Mfalme Nebukadneza nilipata ndoto hii. Sasa, wewe Belteshaza, niambie tafsiri yake, kwasababu hakuna mtu mwenye hekima katika ufalme wangu anayeweza kunitafsiria. Lakini wewe unaweza kufanya hivyo, kwa kuwa roho ya miungu watakatifu iko ndani yako.”

19 Ndipo Danieli aliyeitwa pia Belteshaza, alihuzunishwa kwa muda, na mawazo yake yalimshitua. Mfalme akasema, “ Belteshaza, usifadhaishwe na ndoto au tafsiri yake.” Belteshaza akajibu, “ Bwana wangu, ndoto hii na iwe kwa ajili ya watu wanaokuchukia, na tafsiri yake na iwe kwa ajili ya adui zako.

Read Daniel 4 in the app The whole chapter

Search the Scriptures

Choose a translation

KJVBSBWEBNHEBASVYLTDBYWBTBBEEBRGNVDRALUTCANRIVLSGRVABPMYORIGBSWATGLIRV