The Bible › Biblia Takatifu › Acts 21
Kwa vile Paulo hakutaka kushawishiwa, tuliacha na kusema, “ Basi mapenzi ya Bwana yafanyike.”
Acts 21:14 · Biblia Takatifu
And when he would not be persuaded, we ceased, saying, The will of the Lord be done.
When he would not be dissuaded, we fell silent and said, “The Lord’s will be done.”
When he would not be persuaded, we ceased, saying, “The Lord’s will be done.”
Every translation above is public domain and free to share. Other versions — NIV · ESV · NKJV · NLT · NASB · CSB · AMP — are copyrighted and open on their publishers’ partner site.
11 Yeye alikuja kwetu na akautwaa mkanda wa Paulo. kwa huo alijifunga miguu na mikono yake mwenyewe na kusema, “Roho Mtakatifu asema hivi,” “Wayahudi wa Yerusalemu watamfunga mtu anayemiliki mkanda huu, nao watamkabidhi mikononi mwa watu wa mataifa.”
12 Tuliposikia mambo hayo, sisi na watu waliokuwa wakiishi mahali pale tulimsihi Paulo asipande kwende Yerusalemu.
13 Ndipo Paulo alijibu, “Mnafanya nini, mnalia na kunivunja moyo wangu? Kwa maana niko tayari, siyo tu kufungwa, lakini pia kufia huko Yerusalemu kwa ajili ya jina la Bwana Yesu.”
14 Kwa vile Paulo hakutaka kushawishiwa, tuliacha na kusema, “ Basi mapenzi ya Bwana yafanyike.”
15 Baada ya siku hizi, tulichukua mifuko yetu na tukapanda Yerusalemu.
16 Baadhi ya wanafunzi kutoka Kaisaria pia walifuatana nasi. Wakamleta mtu mmoja aitwaye Mnasoni, mtu wa Kipro, mwanafunzi wa zamani, ambaye tulikaa naye.
17 Tulipofika Yerusalemu, ndugu walitukaribisha kwa furaha.
Read Acts 21 in the app The whole chapter