The Bible › Biblia Takatifu › 2 Samuel 21
Hivyo Daudi akaenda na kuchukua mifupa ya Sauli na mifupa ya Yonathani mwanawe kutoka kwa watu wa Yabeshi Gileadi, waliokuwa wameiiba kutoka katika eneo la jumuiya la Beth Shani, Wafilisti walipokuwa wamewatundika baada ya Wafilisti kumwua Sauli katika Gilboa.
2 Samuel 21:12 · Biblia Takatifu
← PreviousRead 2 Samuel 21Next →
And David went and took the bones of Saul and the bones of Jonathan his son from the men of Jabeshgilead, which had stolen them from the street of Bethshan, where the Philistines had hanged them, when the Philistines had slain Saul in Gilboa:
he went and took the bones of Saul and his son Jonathan from the men of Jabesh-gilead, who had stolen them from the public square of Beth-shan where the Philistines had hung the bodies after they had struck down Saul at Gilboa.
So David went and took the bones of Saul and the bones of Jonathan his son from the men of Jabesh Gilead, who had stolen them from the street of Beth Shan, where the Philistines had hanged them in the day that the Philistines killed Saul in Gilboa;
Every translation above is public domain and free to share. Other versions — NIV · ESV · NKJV · NLT · NASB · CSB · AMP — are copyrighted and open on their publishers’ partner site.
9 Akawaweka katika mikono ya Wagibeoni. Nao wakawatundika juu ya mlima mbele za Bwana, na wote saba wakafa pamoja. Waliuawa katika kipindi cha mavuno, katika siku ya kwanza mwanzoni mwa mavuno ya shayiri.
10 Kisha Rispa, binti Aiya, akachukua nguo ya gunia na akajitanda mwenyewe juu ya mlima kando ya miili ya waliokufa tangu mwanzo wa mavuno mpaka wakati mvua ilipoanza kunyesha. Hakuruhusu ndege wa angani kutua juu ya miili mchana wala ayawani wa mwituni wakati wa usiku.
11 Daudi akaambia alichokifanya Rispa, binti Aiya, suria wa Sauli.
12 Hivyo Daudi akaenda na kuchukua mifupa ya Sauli na mifupa ya Yonathani mwanawe kutoka kwa watu wa Yabeshi Gileadi, waliokuwa wameiiba kutoka katika eneo la jumuiya la Beth Shani, Wafilisti walipokuwa wamewatundika baada ya Wafilisti kumwua Sauli katika Gilboa.
13 Daudi akaiondoa pale mifupa ya Sauli na mifupa ya Yonathani mwanawe, na wakakusanya pia mifupa ya wale watu saba waliotundikwa.
14 Wakaizika mifupa ya Sauli na Yonathani mwanawe huko Zela katika nchi ya Benjamini, katika kaburi la Kishi babaye. Wakafanya kila alichoagiza mfalme. Ndipo Mungu akajibu maombi yao kwa ajili ya nchi.
15 Kisha Wafilisti wakaenda tena katika vita na Israeli. Hivyo Daudi na jeshi lake wakashuka na kupigana na Wafilisti. Akiwa vitani Daudi akachoshwa na vita.
Read 2 Samuel 21 in the app The whole chapter