The Bible › Biblia Takatifu › 2 Peter 2
Maana Mungu hakuwaacha malaika waliokengeuka. Bali aliwatupa kuzimu ili wafungwe minyororo mpaka hukumu itakapowajilia.
2 Peter 2:4 · Biblia Takatifu
← PreviousRead 2 Peter 2Next →
For if God spared not the angels that sinned, but cast them down to hell, and delivered them into chains of darkness, to be reserved unto judgment;
For if God did not spare the angels when they sinned, but cast them deep into hell, placing them in chains of darkness to be held for judgment;
For if God didn’t spare angels when they sinned, but cast them down to Tartarus, and committed them to pits of darkness to be reserved for judgment;
Every translation above is public domain and free to share. Other versions — NIV · ESV · NKJV · NLT · NASB · CSB · AMP — are copyrighted and open on their publishers’ partner site.
1 Manabii wa uongo walijitokeza kwa Waisraeli, na walimu wa uongo watakuja pia kwenu. Kwa siri wataleta mafundisho ya uongo nao watamkana Bwana aliyewanunua. Wanajiletea uharibifu wa haraka juu yao wenyewe.
2 Wengi watafuata njia zao za aibu na kupitia wao wataikufuru njia ya ukweli.
3 Kwa uchoyo watawanyonya watu wakitumia maneno ya uongo Hukumu yao haitachelewa, uharibifu utawafuata.
4 Maana Mungu hakuwaacha malaika waliokengeuka. Bali aliwatupa kuzimu ili wafungwe minyororo mpaka hukumu itakapowajilia.
5 Wala Mungu hakuuvumilia ulimwengu wa zamani. Bali, alimhifadhi Nuhu, mwenye wito wa haki, pamoja na wengine saba, wakati alipoachila gharika juu ya ulimwengu ulioasi.
6 Mungu aliihukumu miji ya Sodoma na Gomora kiasi cha kuwa majivu na uharibifu ili iwe mfano kwa ajili ya waovu katika siku za usoni
7 Lakini alipofanya hilo, alimwokoa Lutu mtu wa haki, aliyekuwa amehuzunishwa na tabia chafu za wasiofuata sheria za Mungu.
Read 2 Peter 2 in the app The whole chapter