The Bible › Biblia Takatifu › 2 Chronicles 28
Kwa kuwa Ahazi aliteka nyara nyumba ya Yahwe na nyumba ya mfalme na viongozi, kwa ajili ya kuvitoa vitu vya thamani kwa mfalme wa Ashuru. Lakini kufanya hivyo hakukumfaidisha yeye.
2 Chronicles 28:21 · Biblia Takatifu
← PreviousRead 2 Chronicles 28Next →
For Ahaz took away a portion out of the house of the LORD, and out of the house of the king, and of the princes, and gave it unto the king of Assyria: but he helped him not.
Although Ahaz had taken a portion from the house of the LORD, from the royal palace, and from the princes and had presented it to the king of Assyria, it did not help him.
For Ahaz took away a portion out of the LORD’s house, and out of the house of the king and of the princes, and gave it to the king of Assyria; but it didn’t help him.
Every translation above is public domain and free to share. Other versions — NIV · ESV · NKJV · NLT · NASB · CSB · AMP — are copyrighted and open on their publishers’ partner site.
18 Wafilisti pia wakavamia miji ya nchi ya chini na ya Negebu ya Yuda. Waliichukua Beth-shemeshi, Ayaloni, Giderothi, SoKo pamoja na vijiji vyake, Timna pamoja na vijiji vyake. Wakaenda kuishi katika sehemu hizo.
19 Kwa kuwa Yahwe aliishusha chini Yuda kwa sababu ya Ahazi, mfalme wa Israeli; kwa maana alikuwa ametenda maovu katika Yuda na alikuwa ametenda dhambi nzito sana dhidi ya Yahwe.
20 Tiglath-pileseri, mfalme wa Ashuru, akaja kwake na akampa tabu badala ya kumpa nguvu.
21 Kwa kuwa Ahazi aliteka nyara nyumba ya Yahwe na nyumba ya mfalme na viongozi, kwa ajili ya kuvitoa vitu vya thamani kwa mfalme wa Ashuru. Lakini kufanya hivyo hakukumfaidisha yeye.
22 Mfalme Ahazi huyu huyu akatenda dhambi hata zaidi dhidi ya Yahwe katika muda wa mateso yake.
23 Kwa maana aliwatolea dhabihu mingu wa Dameski, miungu ambao walimshinda. Akasema, “Kwa sababu miungu wa mfalme wa Aramu waliwasaidia, nitawatolea sadaka ili wanisaidie.” Lakini walikuwa watesi wake na Israeli yote.
24 Ahazi akazikusanya pamoja samani za nyumba ya Mungu na kuzikata vipande vipande. Akaifunga milango ya nyumba ya Yahwe na kuzitengeneza madhabahu kwa ajili yake mwenyewe katika kila kona ya Yerusalemu.
Read 2 Chronicles 28 in the app The whole chapter