The Bible › Biblia Takatifu › 2 Chronicles 2
Lakini ni nani anayeweza kumjengea Mungu nyumba, kama dunia yote na hata mbigu yenyewe haviwezi kumtosha? Mimi ni nani hata nimjengee nyumba, ispokuwa sadaka kwa ajili ya sadaka za kufukiza mbele zake?
2 Chronicles 2:6 · Biblia Takatifu
← PreviousRead 2 Chronicles 2Next →
But who is able to build him an house, seeing the heaven and heaven of heavens cannot contain him? who am I then, that I should build him an house, save only to burn sacrifice before him?
But who is able to build a house for Him, since the heavens, even the highest heavens, cannot contain Him? Who then am I, that I should build a house for Him, except as a place to burn sacrifices before Him?
But who is able to build him a house, since heaven and the heaven of heavens can’t contain him? Who am I then, that I should build him a house, except just to burn incense before him?
Every translation above is public domain and free to share. Other versions — NIV · ESV · NKJV · NLT · NASB · CSB · AMP — are copyrighted and open on their publishers’ partner site.
3 Selemani akatuma ujumbe kwa Hiramu, mfalme wa Tiro, ukisema, “Kama ulivyofanya na Daudi baba yangu, ulivyomtumia magogo ya mierezi ili ajenge nyumba ya kuishi, fanya hivyo hivyo na mimi.
4 Tazama, niko karibu kujenga nyumba kwa ajili ya jina la Yahwe Mungu wangu, kuiweka wakifu kwake, kwa ajili ya kumtolea sadaka za kuteketezwa zenye viungo vitamu mbele zake, kwa ajili ya mkate wa uwepo, na kwa ajili ya sadaka za kuteketezwa asubuhi na jioni, katika siku za Sabato na za mwezi mpya, na katika sikukuu zilizoteuliwa kwa ajili ya Yahwe Mungu wetu. Hii itakuwa milele, kwa Israeli.
5 Nyumba nitakayoijenga itakuwa kubwa sana, maana Mungu wetu ni mkuu kuliko miungu mingine yote.
6 Lakini ni nani anayeweza kumjengea Mungu nyumba, kama dunia yote na hata mbigu yenyewe haviwezi kumtosha? Mimi ni nani hata nimjengee nyumba, ispokuwa sadaka kwa ajili ya sadaka za kufukiza mbele zake?
7 Kwa hiyo nileteeni mtu mwenye ujuzi wa kazi katika kazi ya dhahabu, fedha, shaba, na chuma, na ya dhambarau, na nyekundu, na sufu ya samawati, mtu anayejua kutengeza aina zote za mapambo ya mbao. Atakuwa na watu wenye ustadi waliopamoja nami katika Yuda na Yerusalemu, ambao Daudi baba yangu aliwaweka.
8 Nitumieni pia mierezi, miberoshi, na miti ya msandali kutoka Lebanoni, maana najua ya kuwa watumishi wako wanajua jinsi ya kukata mbao katika Lebanoni. Angalia, watumishi wangu watakuwa na watumishi wako,
9 ili kwamba watayarishe mbao nyingi kwa ajili yangu, maana nyumba ninayotaka kuijenga itakuwa kubwa na ya ajabu.
Read 2 Chronicles 2 in the app The whole chapter