The Bible › Biblia Takatifu › 1 Samuel 21
Sasa basi chakula gani kinapatikana hapa? Nipatie mikate mitano, au chochote kilichopo hapa.”
1 Samuel 21:3 · Biblia Takatifu
← PreviousRead 1 Samuel 21Next →
Now therefore what is under thine hand? give me five loaves of bread in mine hand, or what there is present.
Now then, what do you have on hand? Give me five loaves of bread, or whatever can be found.”
Now therefore what is under your hand? Please give me five loaves of bread in my hand, or whatever is available.”
Every translation above is public domain and free to share. Other versions — NIV · ESV · NKJV · NLT · NASB · CSB · AMP — are copyrighted and open on their publishers’ partner site.
1 Kisha Daudi akafika Nobu kumuona Ahimeleki kuhani. Ahimeleki akaja akutane na Daudi huku akitetemeka na kumwambia, “Kwa nini uko peke yako huna mtu wa kuambatana na wewe?”
2 Daudi akamjibu Ahimeleki kuhani, “Mfalme amenituma kwa jambo maalum na ameniambia hivi, 'Asiwepo hata mtu mmoja anayejua chochote kuhusu shughuli niliyokutuma, na kile nilichokuagiza.' Nimewaelekeza vijana kwenda sehemu fulani.
3 Sasa basi chakula gani kinapatikana hapa? Nipatie mikate mitano, au chochote kilichopo hapa.”
4 Huyo Kuhani alimjibu Daudi na kusema, “Hakuna mkate wa kawaida mkononi, lakini ipo mikate takatifu- kama vijana hawajatembea na wanawake.”
5 Daudi akamjibu kuhani, “Hakika hatujatembea na wanawake kwa siku hizi tatu. Nilipoanza safari, miili ya vijana iliwekwa wakfu kwa BWANA, ingawa ilikuwa safari ya kawaida. Je, si zaidi sana leo miili yao ikawekwa wakfu kwa BWANA.”
6 Hivyo kuhani akampa mikate iliyokuwa imewekwa wakfu kwa BWANA. Maana haikuwepo mikate mingine hapo, isipokuwa tu ile ya wonyesho, ambayo iliondolewa kutoka kwa BWANA, ili sehemu yake iwekwe mikate ya moto, inapokuwa imeondolewa.
Read 1 Samuel 21 in the app The whole chapter